.

8/15/2021

Nandy alamba dili Guinness, Afunguka Sakata la Billnass na Mtoto

NYOTA wa Muziki wa Kizazi kipya, Faustine Mfinanga ‘Nandy’, amewashukuru wadau wa muziki nchini kwa kumshika mkono hadi kufikia kupata mikataba minono.

Akizungumza Dar es Salaam leo Jumamosi Agosti 14, 2021, katika hafla ya kutangazwa kuwa Balozi wa kinywaji cha Guinness Pan Africa, Nandy amesema mafanikio yake yanachangiwa na upendo wa wadau wa muziki.

“Nashukuru uongozi wa Guinness, kwa kunipatia ubalozi katika Pwani ya Afrika naahidi kufanya kazi yangu kwa ufasaha, kikubwaa nawashukuru wadau wa muziki wangu kwa kunishika mkono ndio maana leo hii thamani yangu inazidi kukua,” amesema Nandy

Aidha, Nandy amezungumzia picha ya mtoto ambayo aliweka mpenzi wake Bilinass katika mtandao wa Istagram na kusema kuwa anahisi picha hiyo ni ya mtoto wake.


“Bilinass anapenda watoto, nahisi ile picha itakuwa ya mtoto wake japo yeye mwenyewe haja niambia zaidi ya kufahamu anahitaji mtoto,” amesema Nandy.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger