.

8/30/2021

Roketi tano zarushwa kuelekea kwenye uwanja wa ndege wa Kabul

Roketi kadhaa zilirushwa kuelekea kwenye Uwanja wa ndege wa Kabul mapema leo. Televisheni ya Tolo ya mji wa Kabul imewanukuu walioshuhudia shambulio hilo. 
 
Kwa mujibu wa taarifa makombora hayo yalirushwa kutokea mji wa Chairchanah uliopo kaskazini mwa mji wa Kabul. Hakuna madhara yaliyoripotiwa. 
 
Habari zaidi zinasema mfumo wa ulinzi wa anga ulikuwa umewekwa tayari. Maafisa wa serikali ya Marekani wamefahamisha kuwa mfumo huo ulifanyiwa majaribio wiki iliyopita. 
 
Shirika la televisheni la Marekani, CNN ,limeripoti kwamba hatari iliyokuwepo hapo awali ya uwanja wa ndege wa Kabul kushambuliwa sasa imeondolewa. 
 
Marekani imekamilisha shughuli za kuwaondoa watu na wanajeshi wake wanatarajiwa kuondoka Kabul hapo kesho Jumanne. 
 
Watu wapatao 114,000 wamesafirishwa kwa ndege kutoka Afghanistan tangu katikati ya mwezi Agosti, kulingana na Ikulu ya Marekani.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger