.

8/27/2021

Sakata la Askofu Gwajima lamuibua Rose MuhandoMsanii wa muziki wa Injili Rose Muhando amesema kwamba mvutano unaoendelea kati ya Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima na Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima unapaswa kuangaliwa kwa sura nyingine ili muafaka uweze kupatikana.


Kushoto ni Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima kulia ni Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima

"Askofu Gwajima ni mtumishi wa Mungu na Serikali pia imetoka kwa Mungu, cha msingi ni kuangalia kwa nini hii vita inakuwepo kati ya Gwajima na Serikali au shetani ndiyo yupo hapa katikati," amesema Rose Mhando.

Rose Mhando ameongeza kuwa "Viongozi wa Serikali wanamuhitaji Mungu na viongozi wa makanisa wanaihitaji Serikali, cha kuangalia ni kweli Gwajima anagombana na Gwajima au kuna nini hapa kati, cha kuzingatia ni kwamba tunapigana na muovu hatupigani na Waziri wa Afya wala Mchungaji".


Amemalizia kwa kusema kwamba "Tunaihitaji Serikali pia tunahitaji viongozi wetu wa dini, cha msingi tukae pamoja hili jambo lililotokea lisilete mtafaruku, sisi wote ni watoto wa hapa nyumbani tusimpe ibilisi nafasi".

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger