.

8/19/2021

Vurugu bado zinashuhudiwa katika uwanja wa ndege wa Kabul
Secunder Kermani, mwandishi wetu wa Afghanistan, amekuwa akielezea hali ilivyo huko Kabul.

Anasema bado kuna "vurugu " katika uwanja wa ndege wa jiji hilo wakati Waafghan wanaendelea kujaribu kukimbia kwa ndege za uokoaji, lakini mahali pengine Kabul inaonekana kuwa utulivu zaidi kuliko siku za hivi karibuni wakati biashara zinaanza kufunguliwa.

Mwandishi wetu anasema ni ngumu sana kueleza ukubwa wa uwepo wa Taliban katika mji mkuu, na wapiganaji "wenye silaha kali" wakizunguka jiji kwa miguu na kwa magari.

Anasema benki na ofisi za serikali zinabaki zimefungwa, na wanawake ni wachache wanaoonekana hadharani.

Alisikia pia mlio mkubwa wa risasi kabla ya kuzungumza na kipindi cha BBC Breakfast, lakini akasema chanzo hakijulikani.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger