.

8/06/2021

Waziri Simba Chawene "Wanaowafumania Wapenzi Wakiwa Faragha Kisha Kuwapiga na Kuwarekodi Video Wakamatatwe"


Baada ya kuitazama video inayosambaa ikionesha Mwanaume na Mwanamke wakiwa bila nguo wakipigwa na wanaodai kuwafumania, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata Watuhumiwa waliowashambulia Wapenzi wakiwa kwenye faragha wakidai kuwa wamewafumania.

“Hivi karibuni kumejitokeza tabia ya baadhi ya Watu wanawavamia Wapenzi ambao wanafanya faragha zao, tabia hii ambayo imeshamiri kama clip nyingi zinavyorushwa ni kinyume cha Sheria kabisa kuwaingilia Watu walio kwenye faragha na wakati mwingine wengine kufanya hivyo kwa kisingizio kwamba wamefumania, litakuwa fumanizi kama halijawa jambo la kupanga au Watu kujikusanya na kwenda kuvamia sehemu na pia lazima Mke au Mume awe na cheti halali cha ndoa na sio kusema huyu alikua hawara yangu”

“Wanaodhalilika zaidi katika hili ni Wanawake, wengine wanakuwa uchi wa mnyama hawana nguo wanapata kipigo, naaagiza Polisi Mikoa yote kufuatilia hasa lile tukio linalozunguka kuanzia jana kuhakikisha wanakamatwa na kufikishwa Mahakamani” ——— George Simbachawene.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger