Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Chuo Kikuu Chaanzisha Kozi Ya Drake & The Weekend

CHUO kikuu cha Ryerson kilichopo Toronto, Canada  kimeanzisha kozi ya mastaa wawili watokao nchini humo Aubrey Drake Graham maarufu kama Drake pamoja na Abel Makkonen Tesfaye maarufu kama The Weekend itakayoanza rasmi mwakani 2022.

 

Unaambiwa katika kozi hiyo  wanafunzi wa hapo watajifunza kuhusu rekodi mbalimbali zilizowekwa  na mastaa hao pamoja na safari yao ya muziki kwa ujumla , uongozi wa chuo hicho umethibitisha kuanza kozi hiyo mapema mwakani.

 

Kuna kozi  nyingine  nyingi  zinafundishwa  katika  chuo hicho lakini hii  ni wazi kabisa inaonekana kupendwa na Wanafunzi wengi wa chuoni  hapo, Suala  hili  ni  lakujiuliza  kwa  vyuo  vingi  vya  Afrika  je  kuna  hiki  kitu  ama hakuna , na kama hakuna nini kifanyike dhidi ya suala  hili kwani mataifa yalioendelelea  yanajitanua  katika  nyanja  mbalimbali  na  suala  la  muziki  kuonekana  kama  biashara ama ajira  na  sio  uhuni  kama  ilivyokua  mwanzo .

 

Lakini    ifahamike tu kwamba  haya  maisha  yanaitaji  mfano  wa  kuigwa  watoto  wa  mjini  wanaiita ‘ role  model ” kwa   hivyo   suala   la   wasanii   hawa   wawili kusomwa   katika  chuo  kikuu  ni  chachu kwa vijana wa nchi hiyo , kwa hivyo basi sio mbaya pia hata hapa bongo ikianzishwa kuwasoma wasanii wakubwa ikiwa ni moja ya chachu ya maendeleo kwa vijana.

 

Swali la kizushi je kwa hapa bongo ni wasanii gani utapenda wasomwe katika vyuo vikuu????

 Downlaod App ya BLOG Hii Kutoka Google Play Kwa Kubonyeza HAPA>>>

Post a Comment

0 Comments