Guinea: Wanajeshi Wadaiwa Kumpindua Rais Alpha Conde

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA
Hatima ya Rais wa Guinea Alpha Condé haijulikani wazi baada ya video ambayo haijathibitishwa kumuonyesha mikononi mwa wanajeshi, ambao walisema wamefanya mapinduzi.

Walakini, waziri wa ulinzi amenukuliwa akisema jaribio la kuichukua serikali lilikuwa limeshindwa.

Hii inafuatia masaa mengi ya makabiliano ya risasi karibu na Ikulu ya rais katika mji mkuu, Conakry.

Wanajeshi wa Guinea wamejitokeza katika runinga ya taifa wakithibitisha kwamba rais Alpha Conde ameondolewa madarakani.

Wanajeshi hao wametangaza kuwa nchi hiyo itakuwa chini ya Serikali ya Mpito huku baadhi ya video zikimuonesha Rais Alpha Conde akiwa chini ya Maafisa wa Jeshi.

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad