Ticker

6/recent/ticker-posts

Jela Miaka 30 Kubaka Mhudumu wa Baa
MAHAKAMA ya Wilaya ya Geita imemhukumu mkazi wa Katoro, Justini Silivini (24), kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka.

 

Alitiwa hatiani na kupewa adhabu hiyo baada ya mahakama hiyo kuridhika kuwa alimbaka mwanamke mwenye umri wa miaka 21 na kumsababishia maumivu.

 

Hukumu hiyo ilitolewa Ijumaa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Samuel Maweda, baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha kosa hilo paspo kuacha shaka yoyote.

 

Hakimu Maweda alisema Mahakama hiyo inatoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo ili liwe fundisho kwake na kwa vijana wengine wenye tabia ya kikatili kama yake.

 

Alisema upande wa mashtaka ulipeleka mahakamani shahidi mmoja, ambaye alithibitisha kuwa alibakwa na mshtakiwa huyo.

 

Aidha, Hakimu Maweda alisema mshtakiwa huyo alikwenda kwenye baa iliyopo Mtaa wa Afya Katoro, ambapo mlalamikaji (jina lake limehifadhiwa) anapofanyia kazi.

 

Alisema baada ya mshtakiwa kufika kwenye hiyo baa alimkuta mlalamikaji akiwa anafanya kazi zake, ndipo mshtakiwa huyo alimshika mkono na kumvuta kwa nguvu, huku akiwa na kisu mkononi hadi pembeni mwa baa hiyo na kumvua nguo na kuanza kumbaka.

 

Aidha, alisema mlalamikaji huyo alipiga kelele ndipo wasamaria wema walifika na kumkamata mshtakiwa huyo na kumpeleka katika Kituo cha Polisi Katoro na baada ya mahojiano mshtakiwa alipelekwa katika Mahakama ya Wilaya Geita.

 

Awali akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Clemence Kat, alidai mahakamani kuwa Oktoba 20, mwaka 2020 maeneo ya Katoro Mkoa wa Geita, mshtakiwa alimbaka mwanamke mwenye umri wa miaka 21 na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.


Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments