Wanafunzi wafariki kwa mshtuko wa moyo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Wakazi wa jimbo la Gujarat nchini India wanaendelea kupigwa na mshangao baada ya wanafunzi watatu kufariki ghafla kutokana na mshtuko wa moyo kutokana na mtihani.

Mwanafunzi aliyetambuliwa kwa jina la Sneh alizimia ghafla wakati alipokuwa akifanya mtihani katika shule ya Sekondari ya Limbassi. Baada ya kupelekwa hospitali umauti ulimkuta, madaktari walisema mwanafunzi huyo alifariki kwa mshtuko wa moyo.

Awali katika eneo la Ahmedabad, mwanafunzi aliyejulikana kwajina Sheikh Mohammad Aman Arif aliyekuwa akifanya pia mtihani alianza kuwa na dalili za kuzorota kwa afya yake ambapo gari la kubebea wagonjwa liliitwa na kumkimbiza hospitalini ambako aliongezewa oksijeni lakini alifariki na madaktari walisema shinikizo la damu yake lilikuwa la kiwango cha juu.

Pia, Utsav Shah mwanafunzi mwingine wa sekondari katika shule ya Navsari, alifariki kwa mshtuko wa moyo kabla ya kuanza kufanya mtihani. Watu wa familia yake walimkimbiza hospitalini akiwa na maumivu ya kifua, ambako madaktari walitangaza kuwa amefariki, Baba yake alisema alikuwa na mshituko wa moyo.


 
Vifo vya ghafla vya wanafunzi wanaofanya mtihani wa kitaifa kimewashitua wengi, kwani haijawahi kutokea miaka iliyopita.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad