Majina Wachezaji wa Yanga Yaliyotumwa CAF

KLABU ya Yanga SC imewasilisha majina ya wachezaji 28 waliosajiliwa kwaajili ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu wa 2021/2022 imeelezwa.

 

Klabu hiyo itakayoiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika imepeleka idadi ya wachezaji hao 28 tu waliosajiliwa CAF kwaajili ya michuano hiyo.

 

Kwa upande wa watani zao Simba SC, imeelezwa kuwa wao wamewasilisha orodha ya wachezaji 31 waliowasajili kwaajili ya michuano hiyo ya Klabu Bingwa Afrika.

 

Klabu hiyo ipo kambini ikiendelea kujipanga na mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali ambapo itacheza dhidi ya Rivers United ya Nigeria.

 

Wachezaji hao waliosajiliwa kwaajili ya michuano ya Afrika, upande wa walinda lango wapo watatu (3) ambao ni Diarra Djigui, Erick Johola na Ramadhan Kabwili huku mabeki wakiwa tisa (9) ambao ni Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Yannick Bangala, Dickson Job, Bakari Mwammnyeto.

 

Wengine ni Kibwana Shomari, Djuma Shaban, David Bryson, Adeyun Saleh na Paul Godfrey ‘Boxer’

 

Viungo wapo sita (6) ambao ni Mukoko Tonombe, Khalid Aucho, Feisal Salum Abdallah, Zawadi Mauya, Deus Kaseke, Jesus Muloko na Farid Mussa.

 

Washambuliaji wapo watano (5) ambao ni Fiston Mayele, Heritier Ebenezer Makambo, Yacouba Songne, Said Ntibazonkiza na Yusuf Athuman.

 

Hata hivyo, Yanga itakuwa na nafasi 12 za kuongeza mastaa wengine endapo itafanikiwa kutinga hatua ya makundi ya ligi hiyo baada ya kushindwa kutumia nafasi hiyo katika usajili wa sasa.

 

Yanga itacheza mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United ya Nigeria Jumapili hii ya September 12, 2021 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11:00 jioni na mchezo wa marudiano utafanyika wiki moja baadaye nchini Nigeria.

 

Endapo Yanga itafanikiwa kushinda kwenye michezo yote miwili itakutana na mshindi kati ya Fasil Kenema ya Ethiopia dhidi ya Al Hilal ya Sudan katika hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad