Rais Samia: Wanaosema Huyu Mama Hamna Kitu, Nitaongea nao kwa Kalamu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




KWA mara ya pili Rais Samia Suluhu Hassan amewakemea watumishi wanaodhani kuwa yeye ni mpole na kurudia kusisitiza kuwa ataongea nao kwa kalamu. Anaripoti Patricia Kighono –TUDARCo … (endelea).

Pia ameeleza kukerwa na mameya, wenyeviti madiwani na watumishi wa mamlaka za serikali za miitaa ambao wanagombana, hawashirikiani wala kuheshimiana.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 27 Septemba 2021 wakati akihutubia wajumbe Mkutano Mkuu maalumu wa uchaguzi wa viongozi wakuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT).

“Najua kuna wanaonitizama nilivyo na wakasema huyu mama hamna kitu. Nilisema ndani ya miezi sita nilikuwa nawasoma na ninyi mmenisoma kwa hiyo sasa tumesomana kazi iendelee.”


Amewaambia viongozi hao wanaogombana kwamba wasidhani huko walipo hawaoni.


“Mkurugenzi anasema hili mwingine anasema lile, DC anasema hili DAS wake anasema lile, kuna mivutano na sioni sababu kwanini mvutane, watu mmeamininiwa, mmeteuliwa na mmpelekwa huko kutumikia wananchi. Miongozi kanuni sheria zipo sioni kwanini mnavutana.”

Aidha, amesema sababu ya mvutano huo ni fedha zinapoingia ambapo kila mtu anataka amege fungu lake kwanza atie mfuko kabla ya kwenda kwenye maendeleo ya wananchi lakini pili ni pale mwingine anaposimama kwenye sheria mivutano inaanza.


“Nilisema kwenye mkutano niliyowaapisha mawaziri niliyowabadilisha kuwa sitakaa kwenye viriri kufoka sijaumbwa, sijakuzwa hivyo, mimi yangu kuangalia performance zenu, ambaye ipo chini namwambia waziri sijaridhika na huyu namtoa, watu ni wengine mno wanasubiri hizo nafasi, naweka wengine watakwenda kujituma na kutumikia wananchi.

“Msitegemee nitakuiteni fulani na fulani njooni hapa, kwa nini hivi na hivi! Hapana… wote watu wazima mnayajua mazuri na mabaya, mkifanya mnafanya makusudi nitaongea kwa kalamu narudia tena,” amesema Rais Samia.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad