Ticker

6/recent/ticker-posts

Mbabe: Napumzika ngumi
 
Hilo ni pambano la pili mfululizo Mbabe anachapwa jijini Dar es Salaam, awali alichapwa na Kiduku.
Bondia Abdallah Pazi 'Dullah Mbabe' amesema kwa sasa anapumzika kupanda ulingoni.

Mbabe ametoa kauli hiyo kwenye mahojiano na Mwanaspoti ikiwa ni siku moja baada ya kuchapwa na Alex Kabangu wa DRC.

Bondia huyo namba mbili nchini kwenye uzani wa super middle amesema amelazimika kujipa muda wa kupumzika ili kujipanga upya.

"Mwakani ndio nafikiria nitarudi ulingoni, ila kwa sasa wacha nipumzike kwanza, nitulize akili, nijipange upya ili niwe na ujio mpya nitakaporejea tena ulingoni," amesema.


 
Amesema tangu alipocheza na kuchapwa na Twaha 'Kiduku' Kassim hakupata muda wa kutosha kupumzika.

"Lile pambano nilitumia nguvu nyingi kwenye maandalizi, kabla nilijiandaa pia kwenda kucheza Ujerumani ingawa pambano liliahirishwa, kisha nikacheza na Mcongo.

"Kipindi chote hicho nilitumia nguvu kubwa kuanzia kwenye maandalizi, hivyo nahitaji kupumzika kwanza kipindi hiki," amesema.


Mbabe amewaomba radhi mashabiki wake kwa kipigo cha juzi akisisitiza ni hali ya mchezo.

"Wawe pamoja na mimi kipindi hiki ambacho nitakuwa nje ya ulingo hadi mwakani nitakaporejea tena nikiwa na nguvu na ari mpya," amesema.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments