Mbunge wa Uingereza achomwa kisu na kuuawa kanisani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Mbunge mmoja wa Uingereza kutoka chama cha Conservative cha Waziri Mkuu Boris Johnson amechomwa kisu na kuuawa leo kanisani na mwanaume aliyemshambulia kwenye mkutano na wapiga kura kutoka eneo lake la uwakilishi. 

David Amess, mwenye umri wa miaka 69, mbunge wa eneo la Southend West jimboni Essex, mashariki mwa England, alishambuliwa leo mchana katika mkutano kwenye kanisa la Belfairs Methodist la Leigh-on-Sea. 

Polisi ilivamia kanisa hilo na kusema mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 25 amekamatwa. Wamesema hawamtafuti mtu mwingine yeyote kuhusiana na tukio hilo. 

Wahudumu za dharura walijaribu kuyaokoa maisha yake ndani ya kanisa lakini hawakufanikiwa. Amess ambaye ana mke na watoto watano, alichomwa kisu mara kadhaa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad