Klabu ya Soka ya Simba SC imeibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Magoli ya Simba SC katika mchezo huo uliopigwa jioni ya leo Oktoba 17, 2021 jijini Gaborone yamefungwa na nahodha wa kikosi hicho John Bocco dakika ya pili na sita kipindi cha kwanza.
Mchezo wa mkondo wa pili utapigwa jijini Dar es salaam kwenye dimba la Benjamin Mkapa wiki mbili zijazo. Mshindi wa jumla wa michezo hii miwili atafuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.