Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Mhadhiri anayetuhumiwa kwa rushwa ya ngono Udom aendelea kuchunguzwa

Dodoma. Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kinaendelea na uchunguzi wa tuhuma za rushwa ya ngono inayomkabili mhadhiri wa chuo hicho,  Basil Mswahili.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Oktoba 28,2021 ,  mhadhiri huyo alisimamishwa kazi Oktoba 25,2021 hadi hapo uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo utakapokamilika.

Mswahili ambaye ni mhadhiri katika  ndaki ya sayansi za jamii, jinsia na sanaa katika idara ya lugha za kigeni na fasihi anayefundisha lugha ya Kifaransa alisimamishwa baada ya vikao vya awali vya uongozi wa vyuo hivyo.

Soma zaidi:Udom yamsimamisha mhadhiri kwa tuhuma za ngono

Akizungumza na Mwananchi Digital mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma na masoko katika chuo hicho, Beatrice Baltazary amesema bado mchakato wa uchunguzi unaendelea.

“Bado tunaendelea na uchunguzi kuna kuandika barua na kamati ya nidhamu kujibu na mambo mengine,”amesema.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments