Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Mshambuliaji wa PSG Lionel Messi "Naweza Kurudi Barcelona, Maneno ya Rais wa klabu yaliniumiza"

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Mshambuliaji wa PSG Lionel Messi akihojiwa na chombo kimoja cha habari nchini Uhispania amesema kuwa hakuna aliyemuomba kucheza bure wakati akiwa Barcelona na alikuwa tayari kuisaidia klabu hiyo ndiyo maana aliridhia kupunguzwa asilimia 50 za mshahara wake na anaweza kurejea tena Barcelona.

“Hakuna mtu yoyote kutoka Barcelona aliyeniomba nicheze bure, nilikuwa tayari kupunguziwa 50% ya mshahara wangu na nilikuwa tayari kuisadia klabu hata zaidi ya hapo. Maneno ya Rais wa klabu, Joan Laporta yaliniumiza, sikustahili kabisa.”

Kuhusu kurudi Barcelona? 

“Ndiyo…. Nimekuwa nikisema kila mara kwamba ningependa kuwa na uwezo wa kusaidia klabu. Ningependa kuwa katibu wa mambo ya kiufundi ya klabu (Technical Secretary) wakati fulani, sijui kama itakuwa Barcelona au klabu nyingine, ningependa kujumuika nayo tena,” Lionel Messi.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments