Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Mtoto wa Duterte kugombea umakamo wa rais Ufilipino

Sara Duterte, mtoto wa kike wa rais wa Ufilipino anaemaliza muda wake, anatarajiwa kugombea wadhifa wa makamu wa rais katika uchaguzi ujao wa 2022. 


Awali Meya huyo wa jiji la Davao alitarajiwa kugombea kiti cha urais kwa nia ya kumrithi babake, ambaye anazuiwa kikatiba kuwania muhula wa pili wa miaka sita. Aidha Rodrigo Duterte anakabiliwa na uchunguzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kuhusu hatua kali alizozichukua katika vita alivyovitangaza vya kupambana na madawa ya kulevya nchini mwake. Iwapo atashinda, familia ya Duterte itaendelea kuwa katika wadhifa wa juu wa uongozi, na atakuwa katika nafasi nzuri ya kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2028.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments