Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Polisi yawasaka waliofanya vurugu kanisani Songea

Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma limesema linawasaka watu ambao wanadaiwa kufanya fujo katika kanisa Katoliki Porokia ya Mpitimbi wilayani Songea wakipinga uongozi wa kanisa hilo kukataa kumzika ndugu yao kwa taratibu za kikanisa.


Akizungumza na Mwananchi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Joseph Konyo amesema tukio hilo limetokea Novemba 17, 2021 baada ya Padri wa Parokia hiyo, Dave kugoma kutoa huduma ya mazishi ya aliyekuwa mkazi wa Mpitimbi A, Josefa Komba (30).Kamanda Konyo amesema kuwa ndugu wa Josefa ambaye alifariki dunia Novemba 15, 2021 katika Hospitali ya Misheni Peramiho walikwenda parokoani hapo kuomba ndugu yao azikwe kwa kufata taratibu za kanisa.Amesema kuwa walipofika kanisani walipewa utaratibu kuwa marehemu alikuwa akidaiwa michango kadhaa na walichangishana ili kulipa michango hiyo wakiamini kuwa baada ya kukamilisha ndugu yao atazikwa kwa kufuata taratibu za kanisa hilo.“Walipofika kanisani walipewa utaratibu kuwa marehemu alikuwa akidaiwa michango kadhaa ambapo walikubaliana na utaratibu na kuchangisha na kukamilisha kwa asilimia kubwa wakiwa na matumaini ndugu yao atazikwa kwa heshima za kikatoliki siku ya tarehe 17 Novemba saa sita mchana” amebainisha Kamanda KonyoAmesema kuwa siku ya mazishi asubuhi Padri alipata taarifa kuwa marehemu alikuwa akiishi kinyume na taratibu kanisa hivyo aliuagiza uongozi urudishe michango yao na kueleza kuwa hatatoa huduma ya maziko.“Siku ya mazishi majira ya asubuhi Padri Dave alipata taarifa kuwa marehemu alikuwa akiishi mitala na mume wa mtu hivyo hastahili kuzikwa kikristo ambapo alimuagiza mhasibu aliyefahamika kwa jina moja la Chale arudishe michango yao yote na kueleza kuwa hatatoa huduma ya maziko na kuondoka kwenda mjini Songea kitendo hicho kilileta hudhuni kwa ndugu na waombolezaji hivyo waliamua kuzika bila huduma ya padre” ameelezaKamanda Konyo anasema kitendo hicho kilileta huzuni kwa ndugu na waombolezaji hivyo waliamua kuzika bila huduma ya kanisa.Ameeleza kuwa baada ya maziko watu wasiofahamika waliweka magogo kwenye milango ya kanisa na kuondoka na waombolezaji walipopita kwenye eneo la kanisa hilo walizomea kila mmoja kwa sababu zake.Amesema kuwa Polisi kituo kidogo cha polisi Mpitimbi walifika eneo la tukio na kushirikiana na masista na wanafunzi wa wanafunzi wanaoishi hapo kanisani na kuondoa magogo hayo.Amesema katika vurugu hizo hakuna majeruhi wala uharibifu wa mali yoyote ya kanisa na tayari Jeshi la polisi linaendelea kuwasaka waliofanya vitendo hivyo ili sheria ichukue mkondo wake.Amesema Polisi inawasiliana na uongozi wa kanisa kwa ajili ya kuhakikisha wanakuwa na maelewano kati ya waumini na viongozi wao wa kiroho ili kudumisha amanina utulivu.

 Download Our Udaku Special APP Kutoka Google Play Store Kwa Kutumia Link Hii Hapa>>>

Post a Comment

0 Comments