Rapa Cardi B kutoka Marekani Atimiza Ndoto yake ya Kumiliki Nyumba New York

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Ni wazi kuwa ni ndoto ya kila mja kuwa na maisha mazuri na hilo halipingiki, sasa moja ya ndoto ya muda mrefu ya rapa Cardi B kutoka Marekani, ilikuwa ni kumiliki nyumba jijini New York, ndoto hiyo ameikamilisha ndani ya wiki hii kwa kununua nyumba yake mpya katika jiji hilo.

Cardi B amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa instagram ambapo pia ameeleza kuwa kwasasa ana jumla ya nyumba TATU katika miji tofauti.

"Mimi na mume wangu daima tumekuwa na ndoto ya kuwa na nyumba katika jiji la New York, na tumeamua kuongeza andiko letu kwa kumiliki nyumba. Sasa tuna nyumba Atlanta, Los Angeles (LA) pamoja na New York, ninaweza kuwa na kila kitu nikiwa pamoja na familia yangu wakati wote“ - Unasomeka ujumbe wa @iamcardib.

Caridi B ambaye kwasasa ni mama wa watoto wawili, Kulture Kiari (3) na mtoto wa miezi miwili ambaye jina lake bado halijawekwa wazi, alifunga ndoa na rapa Offset mwaka 2017.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad