Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Sio Masihara Drake Analipa Kodi ya Nyumba Mil. 500/- Kwa Mwezi

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURENYUMBA aliyokuwa anaishi staa wa muziki duniani, Drake, ambayo amehama hivi karibuni, haikuwa ya mchezo kwani kwa mwezi alikuwa analipa kodi ya Dola za Marekani 215,000 (takribani Sh mil. 500 za Tanzania).

Kwa mujibu wa jarida la New York Post, mzaliwa wa Canada huyo anayeishi Marekani analipa kiasi hicho kwenye mjengo wenye ukubwa wa meta za mraba zaidi ya 1672.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Drake aliposti nyumba hiyo hivi karibuni wakati akisherehekea ‘birthday’ yake ya kutimiza umri wa miaka 35.

Jamaa aliishi kwenye nyumba hiyo kwa wiki chache tu kwani hakuwa na mpango wa kuishi hapo muda mrefu kwa kuwa tayari ana mjengo mwingine wa maana nje ya Jiji la Los Angeles.


 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments