Kama ambavyo niliripoti awali, Khalid Aucho ana mkataba wa miaka miwili na Yanga huku Kila kifungu cha mkataba kikitekelezwa vyema pande zote mbili
🔉Ni kweli Aucho alihitajika na klabu zote mbili ila kwake yeye haikuwa kuhusu mafanikio ya Klabu bali maslahi yake binafsi, Yanga walikidhi mahitaji yake ndipo akasaini nao
❌Taarifa za kuwa Simba watamsajili Aucho kwasasa sio za kweli na hakuna Kiongozi yoyote wa Simba aliejaribu kuwasiliana nae kwakuwa bado ana mkataba na Yanga
☑️Lolote linaweza kutokea kama matakwa ya kimkataba hayatotimizwa kama unavyofahamu wachezaji wa Uganda wana elimu kubwa juu ya mikataba, ila mpaka sasa Yanga wanatimiza kwa 100%
🔉Kwasasa Aucho hayupo dimbani kwakuwa anakamilisha program yake ya kurejea uwanjani chini ya Kocha wa Viungo, uwezekano Mkubwa atakuwepo kwenye derby
☑️Ndoa ya Aucho na Yanga ipo imara sana kwasasa Kila Mtu akimfurahia mwenzie
❗Aucho ni moja Kati ya wachezaji wachache sana wanaoishi sehemu ghali zaidi Jijini Dar Es Salaam, kwakuwa ni Professional na amehitaji kuishi maeneo yenye utulivu Mkubwa