Ticker

6/recent/ticker-posts

Marioo ni Mkali Kuliko Diamond Platnumz, Ali Kiba na Hata Harmonize


Mwaka 2021 umeenda vizuri sana kwa upande wa Marioo, kwa ngoma kali alizotoa Inatosha kusema kwamba Marioo ndio muimbaji bora wa kiume Tanzania kwa Mwaka 2021.

Alikiba, Diamond na Harmonize Hawajatoa Hit songs kama ambavyo Marioo kafanya. Mpaka sasa Marioo ndio kawa mfalme wa amapiano Africa mashariki na hili halina ubishi.

Alivyotoa "Mama Amina" mwaka jana mwishoni na ikahit kila kona ya Tanzania, watu walijua amebahatisha, lakini cha ajabu baadhi ya wasanii wa Tanzania wakageuza amapiano ndiyo deal wakaiga na wao wakatoa ngoma kadhaa, ila ikumbukwe marioo ndio mtanzania wa kwanza ambaye ngoma yake ya amapiano ilikuwa hit song kila kona (Mama amina)

Baada ya Mama Amina, Marioo akatoa ngoma kadhaa ambazo sio amapiano na zikafanya vizuri sana then akaamua kuthibitisha kwamba yeye anauwezo mkubwa wa amapiano akadropisha pia "Bia Tamu", wimbo ambao mpaka sasa Sizani kama kuna Mtanzania ambaye haujui kuanzia watoto, vijana, wazee, wanawake, wanaume.

Marioo akaze anakitu ndani yake.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments