WHO: Kirusi Cha Omicron Kinasambaa kwa kasi zaidi ya Delta

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Shirika la afya ulimwenguni WHO limethibitisha kwamba hadi sasa aina mpya ya kirusi cha corona, Omicron inasambaa kwa haraka zaidi kuliko Delta. Kirusi hicho tayari kimeripotiwa katika mataifa 89 ulimwenguni.

Neue COVID-19-Variante Omicron
Kulingana na shirika la WHO bado wanahitajika kukusanya taarifa zaidi ili kupata ufahamu zaidi wa sababu za kirusi hicho cha omicron kusambaa kwa kasi zaidi ya kirusi aina ya Delta. Lakini pia shirika hilo limesema bado kuna taarifa chache kuhusiana na ufanisi wa chanjo dhidi ya corona, na hasa linapokuja suala la aina hiyo mpya ya kirusi.

"Hospitali nchini Uingereza na Afrika Kusini zinazidi kuelemewa na wagonjwa na kutokana na kuongezeka kwa visa vya maambukizi, kuna uwezekano kwamba mifumo mingi ya afya ikaelemewa haraka," limesema shirika hilo.

Wakati shirika la WHO likionya kuhusu kitisho cha omicron, jana Jumamosi, nchini Ujerumani maelfu ya makundi ya watu wanaopinga chanjo pamoja na sera za serikali kuhusu janga la virusi vya corona waliandamana kupinga vizuizi vya kupambana na kusambaa kwa virusi vya corona katika miji kadhaa mikubwa ikiwa ni pamoja na
MMoja ya waandamanaji wanaopinga vizuizi na chanjo nchini Ujerumani.

Polisi ilisema maelfu ya watu waliingia mitaani katika mji wa Hamburg, kaskazini mwa nchi hiyo, na kutembea katika maeneo kadhaa ya katikati ya mji. Takriban watu 8,000 waliandamana baadhi yakiwa na mabango yaliyoandikwa "Hakuna ulazima wa kuchanja" na mengine yakiwa na maneno "msiwaguse watoto wetu".


Nchini Ujerumani kumeanza kutolewa chanjo kwa watoto, baada ya taasisi ya juu ya chanjo kushauri watoto kuchanjwa. Hata hivyo wazazi wanatofautiana kimawazo katika hili.

Katika mji wa Düsseldorf magharibi mwa Ujerumani takriban watu 4,000 waliandamana. Na polisi ilisema takriban watu 3,500 waliandamana katika mji wa Freiburg na wengine katika miji ya Frankfurt, Karlsruhe, Freiburg na Osnabruck, katika jimbo la Lower Saxony.

Mawaziri wa afya Ujerumani wataka hatua kali dhidi ya wasafiri.


Katika hatua nyingine, mawaziri wa afya wa majimbo ya Ujerumani jana Jumamosi walitoa mwito wa hatua kali zaidi kwa watu wanaoingia nchini humo ili kupunguza kasi ya kusambaa kwa kirusi cha omicron, waziri wa afya wa serikali ya shirikisho Karl Lauterbach ameliambia shirika la habari la Ujerumani, DPA baada ya mkutano na mawaziri hao wa kujadiliana kuhusu janga hilo

Bundeskanzler Scholz, erste Regierungserklärung im Bundestag
Serikali mpya ya Ujerumani inataka kila mtu kuchanja kwa lazima, hatua ianyopingwa na baadhi ya wakaazi

Ujerumani imerekodi visa 6,764,188 vya maambukizi na vifo 108,053, hii ikiwa ni kulingana na takwimu za karibuni zaidi kutoka kwa taasisi ya kudhibiti magonjwa nchini humo ya Robert Koch.

Nchini Uingereza hali ni tete wakati kukiripotiwa ongezeko la maambukizi la karibu asilimia 30 kwa wiki hii, huku meya wa London Sadiq Khan akitangaza mzozo huo kuwa ni kama "tukio kubwa".


Ujerumani inataraji kuanzisha vizuizi vya kujitenga kwa wasafiri kutoka Uingereza kuanzia usiku wa kuamkia Jumatatu (20.12.2021) na pia watatakiwa kuonyesha uthibitisho wa kutokuwa na maambukizi wanapoingia nchini humo, hii ikiwa ni kulingana na taasisi ya Robert Koch.

Na Uholanzi inatarajia kuingia kwenye kizuizi kikali cha kufunga shughuli kuanzia Jumapili hii katika kukabiliana na kitisho cha ongezeko la maambukizi ya omicron, hii ni kulingana na waziri mkuu wa mpito Mark Rutte alipozungumza na waandishi wa habari.

Rutte amesema hatua hiyo haikuweza kuzuika kutokana na kitisho cha wimbi la tano lililosababishwa na kirusi cha omicron. Maduka, mikahawa, shule na maeneo mengine ya umma yatalazimika kufungwa katika kipindi hicho. Ni maduka ya bidhaa muhimu tu kama ya supermarkets na maduka ya dawa ambayo hayataguswa na sheria hiyo

Offer ya X Mass Tangaza Biashara yako yoyote Kwenye Blog Hii kwa Sh 10,000 tu

Piga simu 0714604974 kwa Maelezo zaidi
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad