Aliyemuua Mrembo Gesti "Niliambiwa Nimtongoze Alafu Nimuuwe"

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawashikilia Watu wawili wanaodaiwa kula njama na baadaye kumuua Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Barke Pesa Rashid (30) mkazi wa Ilala Utete Jijini Dar es salaam kisa madai ya kwamba Mwanamke huyo aligharamiwa na Mwanaume hadi kumpangishia nyumba lakini akawa na Wanaume wengine.

"Tukio hilo limetokea January Mosi,2022 Tabata Segerea kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo Maridadi ambako tarehe hiyo Mtuhumiwa wa kwanza Mwanaume, Jonsiner Bounser( 34), Mkazi wa Segerea Kalabash Pub alifanya mipango ya mapenzi na Mwanamke aliyemuua baada ya kula njama na Mtuhumiwa mwingine wa pili aliyekamatwa Mwanaume anayeitwa White (33) Mfanyabiashara ya Lori la kuzolea taka Mkazi wa Tabata Segerea"

"Mwanamke huyo alikabwa shingo mpaka kupoteza maisha akiwa katika nyumba hiyo ya kulala wageni, Bounser alikodiwa na White kwa malipo ya Tsh.Milioni 1.7 ili amtongoze na baadaye aende kumuua Mwanamke huyo kwa madai kuwa White alimgharamia sana na kumpangishia nyumba lakini Mwanaume huyo ana Wanaume wengine"

"Bounser amekiri kupewa Tsh. Milioni 1.2 kwa nyakati tofauti kabla na baada ya kutekeleza mauaji hayo na kwamba alikuwa bado anadai Tsh. Laki tano kwa White kwa mauaji ya Mwanamke huyo, uchunguzi wa tukio hilo unakamilishwa na watafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo" ——— Jumanne Muliro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam

Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad