Baba LEVO "Mchumba Hasomeshwi, Penzi la Rayvanny na Paula Taa Nyekundu Imewaka"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Siku ya Jumanne wiki hii kumekuwa na tetesi kemkem ambazo zilisambaa kwa kasi kama moto wa karatasi kwenye ulingo wa burudani kwamba Rayvanny na Paula Kajala wameachana.

Baba Levo kupitia kituo kimoja cha runinga nchini Tanzania amedai kwamba alimuonya Rayvanny kutomlipia ada paula kwenda kusoma nchi za ng'ambo.

“Niseme moja kati ya vitu vimetrendi sana.. ni Rayvanny na Mchumba wake Paula Kajala, naona kama taa nyekundu imewaka. Rayvanny aliniambia anamlipia ada. Mchumba hasomeshwi,” alisema Baba Levo.

Aliendelea kueleza kuwa, “Mabinti wengi wamezoea kula hela za watu halafu wanawakataa.. hata sehemu za baa, ngumi nyingi hutokea kwa sababu hiyo, Mwanamke anaenda analewa pombe ya mtu kisha anatoroka,”

Alipoulizwa kwa nini amesema hayo kuhusu mchumba wa Rayvanny, alidokeza kwamba Rayvanny na paula ni marafiki zangu wakubwa kwenye mtandao wa kijamii.

“Wote ninawafuatilia kama jamaa zangu na marafiki zangu, nimeenda kwenye kurasa zao za mitandao wote wameacha kufuatiliana” alidokeza Baba Levo Na kweli penye moshi hapakosi moto na tunachosubiria nikuona kama watazungumzia mahusiano yao.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad