Mwanaume Mweye Upara Akatwa Kichwa Wakiamini Kina Dhahabu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Polisi nchini Msumbiji wanasema kichwa cha mwanaume mmoja mwenye upara kimekatwa na kuondolewa na wahalifu waliotaka kukiuza kwa mteja wao nchini Mali wakiamini kuwa kina madini ya dhahabu.

Imeelezwa kuwa, mteja wao alitoweka hivyo biashara yao ikabuma na kuamua kukitelekeza kichwa hicho katika mji wa kati wa Muandiwa.

Baadhi ya watu wa Msumbiji wanaamini ushirikina kuwa kichwa cha mwanaume mwenye upara huwa kina dhahabu ndani yake. Ripoti ya kwanza kuhusu kuuawa kwa wanaume wenye upara kwa ajili ya kuchukua vichwa vyao ziliripotiwa mwaka 2017.

Biashara ya viungo vya binadamu ni jambo la kawaida katika nchi za Msumbiji, Malawi na Tanzania ambako vinaaminiwa kuleta utajiri na bahati katika mapenzi. Sehemu za miili ya watu wenye ulemavu wa ngozi (ualbino) huuzwa kwa bei ghali.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad