Waziri Nape Nnauye Aanza Kazi Kwa Kuwafurahisha Watanzania, Aagiza Kusitishwa Upandaji wa Gharama za Internet

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari Mhe. Nnauye Nape ameiagiza TCRA kuyaagiza makampuni ya simu kusitisha upandishaji wa bei ya Vifurushi mpaka hapo watakapokaa na Serikali kuzungumza kuhusu jambo hilo.

Hii imekuja ikiwa ni siku chache tangu wananchi kuanza kulalamikia bei za vifurushi vya simu kupanda ghalfa tena kwa bei kubwa huku wengine wakienda mbali zaidi na kudai kuwa hata kiwango cha vifurushi wanchopewa wakinunua hakiendani na bei hali wanayokuwa wamekatwa.

"Upandaji wa bei za vifurushi limekuwa kama tatizo sugu ambapo mitandao ya simu hupandisha, lakini wakielekezwa na Serikali wanashusha bei, baada ya muda wanapandisha tena.

"Tunaoumia na kuathirika ni sisi wananchi wa hali ya chini, hawa mitandao ya simu ni kama wanatukomoa, tunaomba Serikali iwapangie bei kama ilivyo kwenye mafuta, sukari na bidhaa nyingine badala ya kujipandishia kiholela" amesema Juma Afowe mkazi wa Kibada wakati akizungumza na mtandao huu.

Download App ya Udaku Special BURE Kwenye Simu yako Upate Hizi Habari zetu Kirahisi...Bonyeza HAPA
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad