Alikamwe Mambo 10 nilioyaona Simba Ikiinyoa Prison

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mambo 10 nilioyaona Simba vs Prison

1: Pointi 3 za Alhamdulillah.. Simba inapita kwenye presha kubwa sana, Ndani na nje ya kiwanja.. Jambo zuri kwao wameshinda mchezo mgumu katika siku ambayo hawakuwa bora sana kiwanjani

2: Kuna namna kama shabiki wa soka, Unatamani kuipongeza PRISON kwa Game Plan Yao✊ Tactically walijiandaa vyema kwa kujua Strength za Simba na jinsi ya kuikabili

3: Maswali ni mengi sana kwa Benchi la Ufundi la Simba.. Lakini kubwa, nafikiri matokeo ya nyuma yamewapa presha benchi la Ufundi na inaonekana wamepoteza 'kujiamini' kuanzia kwenye mpango wao wa mechi na 'Selection' ya wachezaji.. Kivipi?

4: Unajua unakwenda kucheza na Prison yenye falsafa ya kudefend kwenye 'Low Block'! Kwanini Simba wanakwenda kuanza mechi na viungo wawili chini [Muzamir & Nyoni]?

5: Unajua unakwenda na Timu yenye sifa ya kudefend katika mstari wa chini, kwanini unachagua kuanza na Sakho kwenye benchi?

6: Tactically ukicheza na timu inayo defend kwenye Low Block unahitaji kucheza na side way passes nyingi kwa ajili ya kuitanua safu yao ulinzi.. Unahitahi pia mchezaji wa pembeni mwenye kasi ya kuingia kwenye half spaces zinapopatikana.. mchezaji mwenye quality ya kushinda 1v1 akiwa kwenye mwendo.. Kwanini SAKHO hakuwa kwenye mpango wa kwanza? Benchi la Ufundi lilipoteza kujiamini

7: Well Done Omary Omary na Marco Mhilu..🙌 Mchango wao kwenye kukaba na kushambulia ulikuwa msingi mzuri wa Prison kupata 'Balance' nzuri wanapokuwa na mpira na wanapoupoteza

8: I Like Bwalya.. Lakini nafikiri anatakiwa kuwa active zaidi kiwanjani. Kasi ya kufikiri na maamuzi ya haraka ni kitu wanachohitaji mastraika wa Simba kudili na mabeki wa Timu pinzani

9: Refa Ahmada Simba.. Nina uhakika kabisa hakuwa na uhakika na maamuzi yake kwenye Lile tukio lililosababisha Penalti. Angekuwa na VAR bila shaka angekuwa na Uamuzi wa Tofauti.. Poor Positioning yake ikamfanya ahukumu kwa kuhisi..

10: Israel Partick Mwenda krosi zake bado kidogo. Ni eneo la kuboresha. Inonga YES.. 👍 Mbangula angeweza kuondoka na bao kipindi cha kwanza kama Henock asingekuwa haraka 'kureact' alipodondoka

Nb: Tajiri namba 15 kaanza kazi 😃
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad