Aliyejinyonga kwa Kuachika Mara Tatu Awaibua Wanaharakati "Alikuwa Bado Mtoto"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Dar es Salaam. Tukio la mtoto wa miaka 17 kujinyonga kutokana na msongo wa mawazo baada ya kuwa anaachwa kila anapoolewa limezua gumzo, ambapo wanaharakati wa haki za waschana wakisema jambo hilo linaonyesha ukubwa wa tatizo la ndoa za utotoni uliopo nchini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amekiri kutokea kwa tukio hilo, akisema msichana huyo aliyetambuliwa kwa jina la Rebecca Benjamini (17) ambaye ni mkazi wa Nyang'hwale mkoani Geita, alikuwa ameachika mara tatu kwenye ndoa.

Mwaibambe amesema hayo jana Februari 17, 2022 alipokutana na Kamati ya Amani na Maadili ya Mkoa wa Geita, ambapo amesema chanzo cha kifo cha Rebecca ni msongo wa mawazo ambao ulikuwa ukisababishwa na yeye kuolewa na kuachika mara kwa mara.

"Rebecca amefariki dunia baada ya kujinyonga hadi kupoteza maisha kwa kutumia kamba iliyosukwa kwa chandarua kwenye kenchi ya nyumba yake, chanzo alikuwa akilalamika kwamba kwanini kila akiolewa anaachika na tayari alikuwa ameshaachika mara tatu," amesema.

Akizungumzia tukio hilo leo Februari 18, 2022 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Msichana Initiative, Rebeca Gyumi anasema sababu za kifo cha mtoto huyo ni msongo wa mawazo ambao umeletwa na athari za kuolewa katika umri mdogo.

Rebecca anasema tukio hilo linaonyesha ni kwa kiasi gani ukatili kwa watoto bado ni mkubwa kwenye jamii, ukosefu wa elimu juu ya madhara ya ndoa za utotoni kuanzia kwenye ngazi ya jamii hadi ngazi za juu bado ni changamoto.

‘’Ukweli kuwa hata baadhi yetu tunavyoliongea hili, hatuliongei katika sura ya ukatili aliopitia kwa huyu binti, ambaye kutokana na tamaduni hizi tunamuona ni mtu mzima, inaonesha tunahitaji mabadiliko kwenye jamii zetu kwa kiasi gani,’’ anasema Rebecca.

Anaongeza kuwa “Rebecca ni mtoto, kama tusingehamasisha tamaduni ambazo hazioni suluhisho la umasikini wetu ni kuoza wasichana au kuona thamani yao inaendana na kuwa kwenye ndoa, yamkini Rebecca asingefika hapa,”
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad