Mastaa Simba wafunguka Mo Dewji kuwa-unfollow

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



BILIONEA wa klabu ya Simba, Mohamed 'MO' Dewji amewachenjia mastaa, makocha na viongozi wa klabu hiyo kwa kuamua kuacha kuwafuatilia (unfollow) kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii.
Mo Dewji aliyeweka udhamini wa mkwanja mrefu katika kikosi hicho hakusema lolote kwanini ameamua kufanya maamuzi hayo tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Kupitia Instagram ya bilionea huyo alibaki na watu 40, ambao ndio atakuwa anawafuatilia ila ndani yake hakuna mchezaji, kocha wala kiongozi wa Simba.

Baadhi ya wachezaji walipata kuzungumza na Mwanaspoti ikiwemo nahodha msaidizi wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, aliyesema hakuwa anafhamu lolote kama kuna jambo hilo limetokea kutoka kwa tajiri wao huyo.
“Wala sifahamu kama kuna jambo kama hilo limefanyika kwa sababu kwetu hakuna mabadiliko yoyote na akili kubwa ni mechi ya kesho (leo),” alisema Tshabalala, huku kiungo Hassan Dilunga alisema si unajua si mtaalamu wa mitandao na suala hilo ndio kwanza nalisikia wakati huu kutoka kwako.

“Bosi si mtu wa mambo mengi sidhani kama kufanya hivyo kutakuwa na adhari yoyote nikuhakikishie hilo,” alisema Dilunga aliyekuwa mchezaji wa mwisho kupostiwa katika Instagram ya Mo Dewji.
Naye Mshambuliaji Chris Mugalu alisema; “Mbona kambini kuna utulivu mkubwa na wala hakuna jambo lolote zaidi kufikiria mechi na Mbeya Kwanza.”

Kiungo Rally Bwalya alisema hayo ni masuala ya mitandao tu kwani wachezaji wote wamefanya mazoezi asubuhi na Hakuna mabadiliko yoyote.

“Mitandao ina mambo mengi, kwangu sioni kama kuna jambo lolote tofauti kama wachezaji tungejua hilo,” alisema Bwalya
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad