Polisi Kuwasaka Waliozusha Katazo la IST na Passo Kupita Daraja la Tanzanite

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Jesho la Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam limekanusha taarifa iliyoambatana na Picha ya Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo Muliro J. Muliro - ACP kuwa amepiga marufuku Magari aina ya IST na PASO kupita katika Daraja jipya la Tanzanite lililopo maeneo ya Surrender Jijini Dar es salaam.

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam linautaka Umma uelewe kuwa halijawahi kutoa Taarifa hiyo inayosambaa kwenye Vyombo mbali mbali vya Habari ikiwemo Mitandao ya kijamii hivyo Taarifa hizo sio za kweli na Jeshi halijajua malengo yake ni nini.

Jeshi linafanya uchunguzi kujua aliyezitoa, kwani hata Milard Ayo amekanusha kuwa ukurasa uliotumika si wake.

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam limeelekeza kuwa halitavumilia kuwepo kwa Mtu/kikundi ambacho kimejikita katika kupotosha Taarifa mbali mbali kwa umma ambapo misingi ya Kisheria itafuatwa ili kuwabaini na kuwafikisha kwenye mamlaka za kisheria watu wanaofanya vitendo hivyo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad