Bilionea Mturuki Ajitokeza Anaitaka ChelseaMFANYABIASHARA na bilionea kutoka Uturuki, Muhsin Bayrak, amepokea ofa ya kutaka kuinunua Klabu ya Chelsea na muda wowote atatua London kukamilisha mchakato huo.

Hii ikiwa ni siku chache baada ya tajiri wa Urusi na mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich kutangaza kuiweka sokoni Chelsea.

Chelsea imewekwa sokoni na dau lake likitajwa kuwa ni pauni bilioni 2.1. Abramovich akiwa na klabu hiyo tangu 2003, amefanikiwa kutwaa mataji 15.

Huyu anakuwa tajiri wa pili kutaka kuinunua klabu hiyo baada ya awali bilionea wa Uswisi, Hansjorg Wyss & LA Dodgers co-owner Todd Boehly kujitokeza kutaka kuinunua Chelsea.


Bayrak ambaye ni bilionea wa Kampuni ya Ujenzi ya AB Grup Holding, amethibitisha kuwa mpango wake wa kutaka kuinunua klabu hiyo.

Taarifa kutoka Uturuki, zimeeleza kuwa: “Imethibitika kuwa ofa imeletwa kwa huyo mfanyabiashara, lakini taarifa nyingine ni siri.”

Mfanyabiashara huyo amezungumza na vyombo vya habari akisema: “Tuko kwenye mazungumzo kuangalia namna ya kuinunua Chelsea tukijadiliana na wanasheria wa Roman Abramovich. Kwa sasa mambo yanayoshughulikiwa ni saini na tutaondoka hapa Uturuki kwenda London wakati wowote kuanzi sasa.”
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad