Kocha Azam Aapa Kutibua Ubingwa Yanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



BAADA ya Jumatano kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Namungo, Kocha Mkuu wa Azam, Abdul Hamid Moallin, ameweka wazi kuwa amefurahishwa na ari na upambanaji wa mastaa wa kikosi hicho na kuapa kuwa anataka kuona wanaendeleza hilo katika kila mchezo, hususani mchezo wao ujao dhidi ya Yanga.

Azam ambayo ilicheza michezo mitatu mfululizo bila matokeo ya ushindi, juzi Jumatano walitoka nyuma kwa bao 1-0 na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Namungo, ushindi ambao umewafanya wapande hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo na pointi 28 walizokusanya kwenye michezo 18.

Baada ya ushindi huo, Azam sasa wanajipanga kuvaana na Yanga ambao wanaonekana kudhamiria kushinda ubingwa msimu huu katika mchezo wao ujao wa ligi kuu, uliopangwa kuchezwa Aprili 6, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Kocha Moallin alisema: “Kwanza kabisa nawapongeza sana wachezaji wangu kwa namna ambavyo walipambana katika mchezo wetu uliopita dhidi ya Namungo, ni wazi ulikuwa mchezo mgumu sana kwetu, nadhani tulikuwa tunakosa upambanaji wa namna hii kwenye michezo yetu iliyopita.


 
“Ninaitaka Azam ninayoifundisha mimi icheze kwa kiwango hiki kwa kila mchezo ulio mbele yetu hususan mchezo dhidi ya Yanga ambao najua ni mchezo mkubwa, lazima tuhakikishe tunatumia faida ya kucheza nyumbani kupata matokeo dhidi yao.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad