Msuva Afunguka "FIFA Wako Pamoja na Mimi, Wameniruhusu Kujiunga na Timu Yoyote Kufanya Mazoezi"NYOTA wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva mwenye mzozo na klabu yake ya Wydad Casablanca ya Morocco, juzi alionekana ametinga uzi wa timu ya Akademi ya Cambiaso dhidi ya Simba na kufunga bao na kuibua maswali kwa mashabiki.

Hata hivyo, mshambuliaji huyo wa zamani wa Moro United na Yanga aliyewahi kucheza Jadid El Difaa ya Morocco amefunguka kuwa, Fifa imempa ruksa ya ya kujiunga na klabu ya kufanya nao mazoezi ili kulinda kipaji chake wakati kesi yake ya Wydad ikiendelea kusubiriwa kuhukumiwa. Ruksa hiyo ndiyo iliyomfanya ajiunge Cambiaso ili kupiga nao tizi, huku akikataa kuzungumza kwa undani juu ya kesi yake iliyopo Fifa na kulishukuru Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuingilia kati.

“TFF ndio kama baba kwa wachezaji, hivyo wapo pamoja nami, Fifa pia tulipopeleka mashtaka wapo pamoja na wachezaji wote wakiangalia haki na kulinda vipaji vyao, kikubwa tusubiri kesi inatoka na majibu gani, nikishindwa sijui itakuaje lakini kama nikishinda basi kuna kiasi kikubwa cha pesa nitapata,” alisema Msuva.

Alisema licha ya kupiga tizi na Cambiaso, lakini baada ya kambi ya Taifa Stars ataenda nje kusaka timu ya kumpa nafasi ya kulinda kipaji chake kwa kucheza mechi za kirafiki. Alipoulizwa kama anaweza kurejea nyumbani kujiunga na timu yoyote, alisema hana mpango wa kucheza soka tena nyumbani licha ya kuwa na matatizo na Wydad.


Msuva yupo nchini kwa muda mrefu baada ya kuwa kwenye mvutano wa kimaslahi na klabu yake na alianza kuhusishwa kujiunga na Simba na Yanga kwa nyakati tofauti.

“Hapana sijafikiria kwa sasa kurudi nyumbani, kuna vitu namalizia halafu nitaondoka kwenda nje lakini sitoenda kusaini kwanza bali nitaenda kufanya mazoezi,” alisema Msuva na kuongeza;

“Nafanya mazoezi yangu lakini naona kabisa hayatoshi na nimekaa nje kama miezi mitatu, nyumbani hapa ukiangalia kila timu kwa sasa wako kwenye mbio za kumaliza Ligi na ndio maana nitaenda nje lakini siwezi kukuambia ni timu gani.”

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad