Samatta aikaribia rekodi ya mabao ya Mrisho Ngassa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta amebakiza mabao 3 kuifikia rekodi ya Mrisho Ngassa ya ufungaji kwenye timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars.
Samatta alifungwa bao 1 kwenye ushindi wa mabao 3-1 walioupata Taifa Stars dhidi ya timu ya taifa ya Jamuhuri ya Afrika ya Kati katika mchezo wa kirafi ulioko kwenye kalenda ya kimataiafa ya FIFA, mchezo uliochezwa uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es salaam jana Machi 23, 2022.

Bao hilo alilofunga ni bao lake la pili anafungwa dhidi ya Afrika ya Kati kwani bao lake la kwanza akiwa na taifa Stars alifunga dhidi ya timu hiyo mwaka 2011. Na bao la jana ni la 22 amefunga akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania katika michezo 60, na kwa sasa Samatta amebakiza mabao 3 kumfikia Mrisho Ngassa mwenye mabao 25 anaetajwa kuwa ndio mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa.

Samatta anaikaribia rekodi hiyo na anaweza kuivunja kabisa kwani Ngassa ameshastaafu kucheza soka, lakini pia katika kalenda hii ya kimataifa ya FIFA Taifa stars inamchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Sudan utakaochezwa Machi 29 2022 na baadae mwaka huu kutakuwa na michezo ya kuwania kufuzu fainali za AFCON hivyo Samatta bado ananafasi kubwa zaidi ya kuweka rekodi mpya.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad