Video Ya Sonia Akiwa Bado Ukraine..

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



WAKATI Serikali ya Tanzania ikiwa imeanza kuchukua hatua za kuwarejesha nchini Watanzania takriban 300 waliopo nchini Ukraine kutokana na hali ya usalama kuendelea kuzorota kwa sababu ya vita na Urusi, binti wa mwigizaji mkongwe wa Bongo Movies, Monalisa aitwaye Sonia Monalisa amewaliza wengi.

Sonia yupo masomoni nchini Ukraine ambapo wiki iliyopita vita nzito imeibuka baada ya Urusi kuivamia nchi hiyo na tayari vimeripotiwa vifo vya mamia wa watu.

Kupitia Mtandao wa Tiktok, Sonia ameachia video ikimuonesha yeye na watu wengine wakiwa wamejikusanya sehemu kama ukumbini wasijue nini cha kufanya baada ya masomo kusimama kutokana na vita. Sonia alikuwa akionesha hali ilivyo akiwa na wenzake ambao ni Waafrika kutokana na rangi zao nyeusi.

Kufuatia video hiyo, watu wengi mtandaoni wamemlilia Sonia kwa kumuandikia maoni mengi ya kumtaka kuwa jasiri huku wakimuombea Mungu amlinde yeye na wenzake na kusababisha kuonekana kama kuna msiba.


Hali bado siyo nzuri hata kidogo kwa sababu hakuna namna ya kutoka kwa sababu anga limefungwa na hakuna usafiri zaidi ya kuwaombea ili hali itengemae na kuwawezesha kurejeshwa nchini.

Katika tamko lake, Serikali ya Tanzania kupitia Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Emanuel Buhohela jana alisema kuwa hatua zinazoendelea kuchukuliwa ni pamoja na kuwaondoa hadi nchi jirani za Poland na Romania ambako kuna utulivu.

“Hatua hii itatoa fursa kuwawezesha raia wetu kurejea nchini kwa usalama,” alisema Buhohela katika taarifa kwa vyombo vya habari.


Hata hivyo, Serikali ilisema hadi jana hakuna Mtanzania aliyepata madhara kutokana na kile kinachoendelea Ukraine
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad