3/19/2022

Wanajeshi Wanne Wa Marekani Wafariki Kwenye Ajali Ya NdegeNdege ya Kivita ya Marekani imeanguka na kuua watu wanne huko Kusini mwa Norway kwenye jimbo la Nordland katika mazoezi ya kivita ya majeshi ya NATO yanayoendelea hadi sasa.

Ndege ya kivita yenye namba MV-22B ambayo ilikuwa chini ya vikosi vya Marekani ilianguka na watu wanne kuthibitika kufariki katika ajari hiyo.


Mkuu wa Polisi wa Nordland Bent Arne Eilertsen aliliambia Shirika la Utangazaji la Umma la NRK kuwa ndege iliharibika vibaya, Alisema: “Tulichoambiwa ni kwamba ni ndege ya Marekani iliyokuwa imebeba wamarekani wanne.”


Marekani na washirika wengine wa NATO wanaendelea na mazoezi ya kivita yaliyopewa jina la “Kukabiliana na baridi 2022” katika ardhi ya Norway eneo lillo umbali wa kilomita chache kutoka mpaka wa nchi hiyo na Urusi.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger