3/19/2022

Msuva Ampotezea Mayele Tuzo ya Mfungaji Bora Msimu huu.
MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva amempotezea kiaina straika wa Yanga, Fiston Mayele na kuwapigia debe George Mpole wa Geita na Reliants Lusajo wa Namungo kubeba tuzo ya Mfungaji Bora msimu huu.

Mayele ana mabao 10 sawa na Lusajo, huku Mpole akiwa nyuma yake na mabao nane, lakini Msuva aliyewahi kunyakua mara mbili Tuzo ya Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara akiwa na Yanga, alisema anatamani kuona wazawa wakitamba mbio hizo.

“Mayele ni mshambuliaji mzuri, ila natamani sana kuona mzawa akiwa mfungaji bora, ligi yetu ina wachezaji wengi wazuri wanaofanya vizuri hivyo namna pekee ya kuthibitisha hilo ni kutwaa tuzo muhimu,” alisema Msuva anayecheza soka la kulipwa Morocco japo ana mgogoro kwa sasa na klabu yake ya Wydad Casablanca.

“Kiukweli, Mpole na Lusajo wapo kwenye viwango bora na naamini mmoja wao anaweza kuwa mfungaji bora kutokana na idadi ya michezo iliyosalia, wanatakiwa kuendelea kukaza buti,” aliongeza Msuva.


Kwa sasa Msuva anaendelea na programu binafsi akisubiri muafaka wa kesi yake na Wydad iliyoko FIFA.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger