3/19/2022

Yanga Wang'aka Kuondoka Mayele Kwenda Kaiser Chiefs

Nafasi za Ajira Jiunge Group la Telegram la AJIRA YAKO Kwa Kubonyeza >> HAPA
Yanga wang'aka kuondoka Mayele
WAKATI kukiibuka tetesi za mshambuliaji hatari wa Yanga, Fiston Mayele kuwaniwa na baadhi ya klabu za nje ya nchi, Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ikitajwa kuwa mojawapo, uongozi wa Yanga umeibuka na kusema hauko tayari kuzungumzia masuala hayo wakati huu wakiwa wamezingatia zaidi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Sasa hivi hakuna dirisha la usajili lililofunguliwa, sasa kwa nini tuanze kuzungumzia habari za usajili sasa hivi? Wengine wanaibuka tu kusema anatakiwa huku na huku, lakini kwa sasa Yanga tunazingatia zaidi kwenye ubingwa hata waseme nani anatakiwa wapi, tunachoangalia sasa ni ubingwa ndipo tunapopazingatia zaidi kwa sasa,” alisema Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli.

Mayele ambaye ametua Yanga msimu huu amekuwa moto wa kuotea mbali kwa namna ya uchezaji wake, lakini pia akiongoza orodha ya wafungaji bora mpaka sasa akiwa amefunga mabao 10 sawa na Reliants Lusajo wa Namungo.

Yanga yenyewe pia inaongoza ligi kwa pointi 45 ikifuatiwa na Simba yenye pointi 37 baada ya mechi 17. Yanga inapambana kutwaa ubingwa huo, baada ya kuukosa kwa misimu minne mfululizo wakilishuhudia likitua Simba
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger