3/19/2022

Hamisa Achezea Levo za Hatari Marekani
HAMISA Mobeto; ni mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania aliye pia msanii wa Bongo Fleva ambaye wiki hii amethibitisha siyo wa mchezomchezo baada ya kuchezea levo za hatari nchini Marekani aliko kwa sasa.

Habari za ndani zinaeleza kwamba, Hamisa yupo New York nchini Marekani ambapo amekwenda kukutana na mkurugenzi wa kinywaji maarufu duniani ambacho amekuwa balozi wake kwa muda mrefu sasa kwa ukanda wa Afrika.

Akiwa nchini Marekani na meneja wake, Mangoma Hamisa amefikia hoteli ya kifahari jijini New York ambapo anaonekana akichukuliwa na gari la kifahari kisha kupelekwa kwenye ofisi za makao makuu ya kinywaji hicho kisha kuonana na mkurugenzi wake.

Mbali na kutembelea ofisi hizo, pia atakwenda kumtembelea ‘mtu wake’ wa karibu nchini humo ambaye ni rapa wa kiwango cha Dunia, Rick Ross mwenye maskani yake, Miami nchini Marekani kwa ajili ya mipango yao mingine ambayo jamaa huyo alishakiri kwamba ana ‘koneksheni’ anazofanya na Hamisa.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger