4/23/2022

Country Boy Alipoteza Muda Sana Pale Konde Gang Kwa HarmonizeMara baaada ya msanii wa muziki Bongo, Country Boy kuachana na Konde Music worldwide miezi mitatu iliyopita amefanikiwa kufungua lebo yake ya muziki na kuipa jina la Ia I Am Music.

🍁Chini kile alichoandika Country Boy kuhusu lebo hiyo;

"Rais wetu mpendwa, Mama etu kipenzi MH SAMIA SULUHU HASSAN kuhakikisha Nchi yetu inasonga mbele mimi kama kijana sijataka kubaki nyuma.

Nimefungua kampuni iitwayo @iam_music_co ambayo itahusika katika kusaidia vijana Mtaani ambao wengi wanataman kutimiza ndoto zao lakini wanashindwa kutimiza kutokana Na changamoto wanazokutana nazo hvyo basi Nakuja mbele yenu Watanzania na serikali kwa ujumla kuipokea KAMPUNI hii.

Hatuna pesa nyingi lakin Tunaamin katika kidogo tulichonacho Kitatuvusha kutoka sehem Moja kwenda Nyingne🙏🏿"

🍁Ukiachana na swala la kufungua lebo yake mwenyewe, Country boy wa nje ya kondegang kapata mafanikio kimuziki zaidi ya alivyo kuwa kondegang

🍁Kwa muda county boy amekuwa chini ya kondegang hakuwahi fanya movements kubwa kimuziki, muziki wake haukusikika na kama asingetoka basi angepotea kabisa

🍁Hii inaleta picha ya kwamba hata killy na cheed wanapotezewa muda tu pale kondegang, hakuna cha maana wanachofanyiwa

Msumbufu

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger