4/20/2022

Diamond Platnumz sio Mwenzetu, Yeye na Rihanna Kwenye Wimbo MmojaDiamond platnumz amefunguka kuhusu matamanio yake pamoja na jitihada ambazo yeye na uongozi wake wamezifanya kwaajili ya kumshirikisha msaniii maarufu duniani Robyn Fenty maarufu Rihanna kwenye moja ya wimbo wake utakaopatikana kwenye album yake ijayo.

Nyota huyo ameyasema hayo alipokuwa kwenye mahojiano maalum na BBC wakati wa Listening part yake iliyofanyika huko London, baada ya kuulizwa na mtangazaji kuhusu msanii ambaye hajawahi kushirikiana naye na angependa siku moja wafanye kazi pamoja.

“Ningependa kufanya kazi na Rihanna, kwa sababu nahisi kwa pamoja tunaweza kufanya ngoma nzuri, Natumaini kama sio kwenye album hii basi album yangu itakayofuata Tunaweza kuwa tumefanya kazi kwa sababu kila kitu kimekwisha shughulikiwa.

Tumeshazungumza na Rihanna pamoja na timu yake na kila kitu kipo sawa nadhani tangu mwaka jana kama sijakosea.”

Mwanamuziki huyo anayefanya vizuri na EP yake mpya ‘FOA’ amesema kuwa kolabo hiyo kama itafanikiwa kwa wakati pengine ikapatikana katika album yake anayotarajia kuitoa siku za usoni na kama itashindikana basi itakuja kwenye album nyingine baada ya hiyo.

Diamond kwa sasa yuko nchini Uingereza alikokwenda kwa ajili ya kufanya ziara kwa vyombo mbali mbali vya habari kama sehemu ya kuendelea kuitangaza zaidi EP yake mpya ‘FOA’.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger