4/20/2022

Frederick Mwakalebela "Hakuna Ubishi SIMBA Wanaenda Kutupa Ubingwa"


MAKAMU Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, amesema mchezo wao wa Dabi ya Kiriakoo dhidi ya Simba, utakuwa ni maalumu kwa wao kutangaza ubingwa wao na baada ya hapo watataja mikoa ambayo kombe lao litapita.

Akizungumza na Championi Jumatano, Mwakalebela alisema, tayari Yanga imeshafanya maandalizi ya kutangaza ubingwa kuelekea Aprili 30, mwaka huu, japo wamesikia kuna fununu kuwa Simba wameomba mchezo huo kusogezwa mbele.

Mwakalebela alisema kwamba, pamoja na maombi yao hayo ambayo hayajawekwa wazi, anachokijua yeye ni kwamba hata kama mchezo ukisogezwa mbele kubwa wafahamu tu kwamba, wakikutana itakuwa ni siku yao maalum ya kutangaza mikoa na mitaa ambapo kombe hilo watalipitisha baada ya kukabidhiwa na TFF.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger