Hanscan Afunguka Changamoto Kufanya Video za Collabo


Unapozungumzia kukua kwa soko la muziki nchini moja kwa moja unamgusa msanii ambaye ndiye anayejulikana lakini kwa walio wengi wamekuwa wakimuacha mwongozaji wa video (wasanii) ambaye pia ni nguzo ya muziki kwa maana anamwongoza msanii kwenye kazi yake mpaka kukamilisha video ya wimbo husika.

Licha ya kuwa kuna mengi nyuma ya pazia katika uandaaji wa video za muziki ambazo waongozaji wa video huzipitia hadi kukamilisha kazi zao, mengi yamekuwa hayasemwi. Sasa mwongozaji mahiri wa video nchini @hanscana_ amefunguka CHANGAMOTO kubwa kushoot video za kolabo.

Kupitia insta story yake @hanscana_ amefunguka kuhusu hilo akieleza kwamba "Kuna mmoja (msanii) anakuwa hayupo serious na uwekezaji wa mwenzie so anaweza fika set muda anaotaka na kuwaendesha vile anavojisikia yeye anasahau kuwa mwenzie asa hela na anachofanya ni kumtia hasara pasina sababu za msingi''

@hanscana_ aliyewahi kuongoza video mbalimbali ikiwemo "Mwambieni" ya msanii Zuchu, ameongeza kuwa, "Kuna hii sentensi imetengeneza masikini wengi sana jiepusha nayo 'I DO WAT I LIKE'.
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad