4/23/2022

Johnny Depp adai hata angepewa offer ya $300 milion, hawezi kuwa tena Jack Sparrow

 


Najua wengi wenu wapenzi wa franchise ya The pirates of the carribean.


Na najua bila shaka mnaipenda kwasababu ya Captain Jack Sparrow ambayo ni character inayochezwa na Johnny Depp.


Ila kwanza watengeneza movie walikuwa washaamua kwamba hatahusika tena katika movie hiyo kutokana na scandal alizonazo ikiwemo matumizi ya madawa na unyanyasaji. Haya yote yameibuka kutokana na mgogoro unaoendelea baina yake na aliyekuwa mke wake Amber Heard.


Amber Heard ambaye mwaka juzi inasemekana alikuwa na mahusiano na Bwana Elon Musk pia ni mcheza movie mashuhuri. Kabla ya kuachana walikuwa katika ugomvi mkubwa huku kila mmoja akimwinda mwenzake kupata ushahidi wa makosa anayofanya.


Ilifika kipindi wanategesheana hadi camera za siri, vinasa sauti, mwingine anamprovoke mwenzake alipuke amrekodi.


Kuna hadi picha za kinyesi kitandani ambapo kila mmoja anasema aliyekiporomosha ni mwenzake.


Mgogoro umeenda mbele zaidi ambapo sasa Johnny alifungua madai akitaka Amber amlipe $50 kwa kuchafua jina lake nje ya makubaliano yao kuwa baada ya taraka hawatazungumzia yaliyotokea kwenye ndoa.


Sasa akiwa mahakamani alisema kuwa hata angepewa ofa ya $300 milion dollars, asingekubali kucheza tena filamu ya pirates of the carribean. Ila wakili alimuonyesha ushahidi kuwa watengeneza Movie wenyewe walishasema kuwa hatohusika tena, yeye akajibu hakuwa na taarifa hiyo.


Johnny inadaiwa aliingiza kiasi $650 kutokana na movie hizo.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger