Kijana Afikishwa Mahakamani Kwa Tuhuma za Kukata Viuno Hadharani


Maulid Hussein Abdallah, mkazi wa Kijiji cha Mwera Wilaya ya Magharibi Unguja visiwani Zanzibar, amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kukata viuno hadharani.

Kijana huyo anatuhumiwa kutenda kosa hilo katika Mji wa Kibole, Wilaya
ya Kati, Kusini Unguja majira ya saa 11 jioni ambapo inaelezwa kwamba akiwa amevalia mtandio, alianza kucheza kwa kukata viuno hadharani, jambo ambalo ni kosa la kisheria visiwani humo.

Mshitakiwa huyo amepinga mashtaka hayo na kuiomba mahakama kumpa
dhamana kwa kuwa yupo kituo cha polisi siku nyingi.

Amri ya kupelekwa rumande imetolewa na Hakimu Safia Waziri, baada ya
mshitakiwa kushindwa kutekeleza masharti ya dhamana ambayo yalimtaka kuwa na mdhamini mmoja ambaye atasaini bondi ya TZS 100,000 pamoja na barua zikiambatana na kopi ya kitambulisho cha Mzanzibar.

Mshitakiwa baada ya kushindwa kutekeleza masharti hayo, mahakama iliamuru arudishwe mahabusu hadi Aprili 25, mwaka huu kwa ajili ya kuanza
kusikiliza ushahidi.
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad