Kocha Orlando Aihofia Simba kwa Mkapa, Kukutana na Wakati Mgumu wa Mashabiki Elfu 60,000KOCHA Mkuu wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Josef Zinnbauer amesema kuwa ubora wa Simba na matokeo mazuri waliyoyapata katika michezo ya Kombe la Shirikisho msimu huu yanawapa mawazo ya kuwatambua kuwa timu hiyo ni imara haswa inapokuwa katika uwanja wake wa nyumbani.


Orlando Pirates wanatarajiwa kuwa wageni wa Simba katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika Aprili 17 katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Kocha huyo aliweka wazi juu ya hofu yao na ubora wa Simba wanapokuwa katika uwanja wao wa nyumbani jambo ambalo linamfanya akiri kuwa wanatarajia kuwa na mchezo mgumu dhidi ya Simba japo wapo tayari kwa mapambano.


Wachezaji wa Orlando Pirates

“Simba katika hatua ya makundi wamepata ushindi katika michezo yao yote ambayo wamecheza nyumbani, rekodi yao pia wanapokuwa katika uwanja wao imekuwa ni nzuri hivyo utaona kabisa mchezo wetu dhidi yao utakavyokuwa.

 

“Kwetu sisi ni furaha kuona tutapata ushindi dhidi yao pamoja na rekodi na ubora wao lakini pia na sisi tuna upande wetu na sidhani kama itakuwa ni mechi ya upande mmoja pekee, bali ni pande mbili za mapambano haswa ya mpira,” alisema kocha huyo.

 

Orlando wanatarajia kukutana na wakati mgumu kwenye mechi hiyo kwenye Uwanja wa Mkapa, baada ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kuiruhusu Simba kuingiza mashabiki elfu 60,000 kutoka elfu 35,000 ambao walikuwa wakiingiza kwenye mechi zao za hatua ya makundi.
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad