4/22/2022

Maboss wa Facebook na Whats App Wakaa Meza Moja na Viongozi wa TRA Tanzania Kuona Jinsi Gani Watalipa Kodi


Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza majadiliano na Kampuni ya Meta inayomiliki mitandao ya Facebookapp, Instagram na Twitter kwa lengo la kuanza kukusanya kodi katika kidijitali kupitia huduma zake nchini.


TRA jana Alhamisi Aprili 21, 2022 ilitoa taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Twitter ikieleza kufanya mazungumzo hayo jijini Dar es Salaam.


“Timu ya wataalamu wa Kampuni ya @meta inayomiliki mitandao ya @facebookapp @instagram pamoja na @whatsApp leo 21 Aprili, 2022 imefanya mazungumzo ya awali na TRA kuhusu namna ya kutoza kodi katika huduma zao nchini,” imeandika katika ukurasa huo wa TRA.Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA, Richard Kayombo alipoulizwa alisema mazungumzo hayo yanalenga mpango wa Serikali kuanza ukusanyaji wa kodi katika huduma wanazotoa hapa nchini.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger