4/23/2022

Martin Kadinda Afunguka Kuhusu Wema Sepetu Kumfukuza Lulu Michael na Wolper Kwake


Baada ya video kusambaa Wema Sepetu kwa hasira akiwafukuza nyumbani kwake Irene Uwoya na Lulu Elizabeth Michael na watu kujiuliza kulikoni, Martin Kadinda afunguka

Mastaa waliofika kwa Wema walikuwa ni Irene Uwoya, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Aunt Ezekiel, Kajala, Jaquline Wolper

Kutokana na hilo kuliiubuka malumbano jambo lililowalazimu mastaa wengine akiwemo, Martin Kadinda kuingilia kati na kuwataka wasiondoke huku akionekana kumrudisha Lulu kwenye kiti ambaye alikuwa ameinuka tayari kwa kuondoka.

“Kilichotokea ni kama hivyo mlivyoona kuliibuka mabishano baada ya sisi kutaka kuwakutanisha mastaa hao ili kumaliza tofauti zao ambazo kwa kiasi kikubwa sisi tunaona wanatengenezewa na wapambe na sio kweli kuwa wana bifu,” Martin Kadinda ameliambia Mwananchi

“Tulimwambia Wema kuwa kuna wageni wawili watakuja siku ya leo, lakini alikuwa anajua ni Wolper na Kajala, hivyo alipotoka na kuwaona ni wakina Lulu, ndio akapanik na kuwataka waondoke.

‘Ila namjua vizuri Wema ni mtu wa kupanik lakini naamini baadaye atakuja kuona alichokifanya sicho na mambo yatakaa sawa kama ambavyo tunatamani iwe kwani ukweli ni kwamba watu hawa hawana ugomvi wowote ila watu wan je ndio wanawatengenezea bifu hizo ambazo hazina faida kwao zaidi ya kuwanyima madili,”amesema

Awali Wema aliingia kwenye bifu na Lulu baada ya Wema kupitia app yake kufanya interview kumuuliza Mama Kanumba baadhi ya maswali ili hali kesi ya Kanumba na Lulu ilishaisha na Lulu kutumikia adhabu na baadaye kutoka, hata hivyo haijulikani Kama walipatana au vipi kwani wiki kadhaa zilizopita wakati Aristotee alipomsema Wema kuwa hana gari na kuwa gumzo, Lulu aliandika post ya kumtetea Wema

Kuhusu Wema na Uwoya waliwahi kuingia kwenye vita baridi wakati wa tuzo flani kwahiyo haijulikani Kama waliyamaliza vizuri na hao watu wao wa karibu yao ndio wanaowagombanisha kama alivyosema Kadinda, Kama Kuna sababu nyingine au lah!

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger