Msajili Akionya Chama Kipya cha Umoja Party

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, amesema ni kosa kisheria kwa chama cha siasa kilichowasilisha maombi ya usajili wa muda kufanya kazi kabla ya kupewa cheti cha usajili huo.

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza alieleza hayo jana katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyokemea chama cha siasa cha Umoja Party kinachodaiwa kuanza kazi za siasa kabla ya kupewa cheti cha usajili wa muda.

Nyahoza alinukuu kifungu cha Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258 kifungu kidogo cha 7(3) kinachoeleza kuwa “hakuna taasisi itakayofanya kazi kama chama cha siasa hadi kiwe kimesajiliwa kwa mujibu wa sheria.”

Taarifa hiyo ilieleza kuwa chama cha siasa cha Umoja Party kimewasilisha maombi ya usajili wa muda na kwa sasa yanafanyiwa kazi hivyo hakipaswi kuanza shughuli za siasa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo katika mitandao ya kijamii kulikuwa na picha zikiwaonesha wafuasi wanaosemekana kuwa ni wanachama wa chama hicho wakiwa wamevaa sare ya fulana zenye bendera ya chama na picha ya kiongozi ambaye si mwanachama wao.

Nyahoza alisema ni kosa kisheria kutengeneza na kuvaa fulana hizo kwa wanachana na Watanzania wote kwa ujumla na kuwataka kuacha kuzivaa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad